About


Sisi ni timu ya marafiq tulioamua kujiunga pamoja na kuongelea kuhusu chakula na vyakula. Kuanzia upatikanaji wake, yaani iwe sokoni, maduka makubwa (yaani supermarket), gengeni na kadhalika. Tutaongelea umuhimu wa vyakula ndani ya miili yetu, je tunapata virutubisho na madini gani, kwanini tunywe maji mengi, au kwanini tule mlo flani. Tutashauri kutoka kwa ushirikiano na maelekezo kutoka wa wataalamu kujuza marafiq wengine je, ni chakula gani wakile au watayarishiwe wale rafiqs wanaosumbuliwa na magonjwa tofauti tofauti.


Tutaenda mpaka kuangalia je, ni chakula gani bora kwa mama wajawazito, chakula gani ni bora zaidi katika ukuaji wa mtoto, maana ni vyema kuijenga afya na akili ya mtoto toka udogoni, na tutaongelea mengineyo mengi ambapo utaalamu huo utapatikana kutoka kwa vyanzo vya uhakika kabisa tukimaanisha waganga waaminifu na waliohitimu stashahada ya uganga.

Tutafundisha namna ya kupika vyakula mbalimbali tukianzia vya hapa hapa nyumbani hadi vya wenzetu wa nje ya bara la Afrika tunaongelea nchi kama za Italy, India, China na kadhalika kwa kupokea mafunzo kutoka kwa marafiq mbalimbali toka pande mbalimbali.
Mbali na hilo tutaonesha ubunifu mbalimbali ambapo tunaongelea njia mbadala zitumikazo iwapo chombo ambacho tumezoea kutumia mara kwa mara hakipo au kina hitilafu. Ubunifu huu tutautoa toka pande mbalimbali tunazotembelea na kukuta na rafiqs wenzetu ambao wanazitumia na zina wasaidia katika njia moja au nyingine
Tutaonesha na kukujuza maeneo mbalimbali zilipo restauranta, migahawa na magenge ya kuuzia chakula yaliyopo nje na ndani ya Dar Es salaama na Tanzania.
Karibuni sana!!
 Na sasa tunapika na kuuza vyakula mbalimbali kwenye sherehe mbalimbali, wasiliana nasi kuweza kujua bei zetu na aina ya vyakula tunapika. 


TAHADHARI: VYAKULA VYA AINA VYOTE VITAONESHWA NDANI YA BLOG HII !!!.